Semina ya namna ya kutumia vifaa vya tahadhari na zimamoto

Maoni katika picha
Kitengo cha usimamizi wa kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimetoa mafunzo ya namna ya kutumia vifaa vya tahadhari na zimamoto, kwa watumishi wa vitengo tofauti na wapiganaji wa kikosi cha Abbasi (a.s), ikiwa kama sehemu ya kuwajengea uwezo wa kupambana na majanga ya moto kwa kutumia njia sahihi.

Semina ilikua ya siku saba, kila siku ilikua na saa nne za masomo, wamesomeshwa mambo mengi, ikiwa ni pamoja na namna ya kupambana na moto na namna ya kutumia vifaa vya kutoa tahadhari, wamefundishwa pia namna ya kutumia zimamoto kwa mikono na namna ya kuzima moto mdogo na mkubwa.

Mkufunzi mkuu wa semina hiyo Ustadh Salaam Alawi Abbasi ameongea na mtandao wa Alkafeel kuhusu semina hii kua: “Ni muhimu sana washiriki wa semina hii watambue namna ya kuamiliana na moto na wajue matumizi ya vifaa vya kutumia kwa mikono, ni muhimu sana kila nyumba iwe na vifaa vya kuzimia moto kwa ajili ya usalama, ongezeko la kiwango cha joto kimataifa na uzembe katika kutumia vifaa vya umeme ni sababu ya kuwepo kwa matukio ya moto yasiyo tarajiwa, janga la moto husababisha maafa –Allah atuepushie- ndipo tukaamua kufanya semina hii ambayo tumefundisha kwa nadhariya na vitendo”.

Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya tukufu hutoa semina na mafunzo mbalimbali kwa watumishi wake kutoka vitengo tofauti, na hutumia wakufunzi mahiri walio bobea katika sekta mbalimbali, kwa ajili ya kuwanoa zaidi watumishi na kuwawezesha kutoa huduma bora ndani na nje ya Ataba tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: