Atabatu Abbasiyya tukufu imehuisha moja katika athari za muhakiki (Ibun Mutwahari Hilliy) ya kifiqhi.

Maoni katika picha
Hivi karibuni kituo cha turathi za Hilla chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu cha Atabatu Abbasiyya tukufu kimetoa kitabu cha Fiqhi kutokana na athari za Shekh Muhammad Hilliy maarufu kwa jina la (Fahari ya wahakiki na Ibun Allaamah Hilliy) ambacho kimechapishwa kwa mara ya kwanza, kimetokana na orotha ya nakala kale za Hilla zilizo hakikiwa ambazo ndio msingi wa machapisho ya kituo, kazi hiyo inaonyesha kuzijali turathi za zamani na wasomi wa Dini, hakika athari walizo ziacha zina mchango mkubwa wa kuhuisha mafundisho ya Dini na kubakisha fikra zao na kutimiza malengo yao, hilo ndio kusudio la wenye akili katika kila umma, na kuonyesha kuzijali athari za wasomi wa Dini.

Kitabu hicho kimepewa jina la: (Mas-ala tofauti ya kifiqihi yaliyo andikwa na fahari wa wahakiki Ibun Mutwahari Hilliy) nacho kimetokana na uhakiki wa Shekh Qassim Ibrahim Alkhaqani, na kukaguliwa na kituo cha turathi za Hilla, kimekusanya kimekusanya mas-ala ya kifiqhi pamoja na mambo mengine (209) yaliyo andikwa katika juzu mbili.

Shekh Muhammad Hilliy anajulikana kwa jina la (Fahari ya wahakiki na Ibun Allaamah Hilliy) ni Shekh Abu Twalib Muhammad bun Shekh Hassan bun Yusufu Alhilliy maarufu kwa jina la Fahari ya wahakiki Ibun Allaamah Alhilliy, Shekh Ibun Daudi Alhilliy katika kitabu chake cha Rijali amesema kua ni: (Shekh wa taifa na Allaamah wa zama zake, mhakiki na mdadisi, anavitabu vingi, katika uongozi wake kwenye madhehebu ya Imamiyya aliandika kitabu cha Ma’aquul na Manquul), naye Shahidi wa kwanza akasema kua: “Shekh alikua ni kiongozi na mfalme wa wanachuoni, kilele cha utukufu, mwisho wa mamujtahidi na fahari ya Dini…”.

Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya tukufu inaipa umuhimu mkubwa kazi ya kuhakiki vitabu na nakala kale, na kuzichapisha upya katika muonekano mzuri, hadi sasa wamesha chapisha mamia ya vitabu vilivyo hakikiwa na vimekua kimbilio la watafiti na wasomi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: