Katika siku kama ya leo (22 Juni) mwaka wa (2014m) ulitekelezwa wajibu wa kisheria na kitaifa kuhusu nchi na maeneo matakatifu, ikiwa ni sehemu ya mwitikio wa fatwa ya Marjaa Dini mkuu ya wajibu kifaya ya kulinda ardhi ya Iraq na maeneo matakatifu, lilitolewa tangazo la kuundwa kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji, ndani ya jengo la Alqamiy la mazuwaru chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu.
Tangazo lilitolewa na rais wa baraza la mkoa wa Karbala Ustadh Naswifu Jaasim Khatwabi, alisema kua: “Katika kuitikia wito wa Marjaa, na kutokana na kuongezeka idadi ya watu wanaojitolea katika mkoa huu, na vituo vilivyopo kushindwa kuwachukua wote, kamati ya Hashdi Sha’abi ya mkoa huu chini ya kanuni na vigezo vya wizara ya ulinzi imeamua kufungua vituo vipya kwa ajili ya kupokea wanao jitolea kwenda kupigana chini ya uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya”.
Akaongeza kua: “Hakika vituo hivyo ndio msingi wa kuunda kikosi cha ulinzi wa taifa ambacho kinaitwa (kikosi cha Abbasi –a.s-).
Akasema: “Watu wanaokuja kujiunga wataingizwa katika vikosi vya askari, watapigana chini ya usimamizi wa jeshi la serikali, kama alivyo elekeza Marjaa Dini mkuu Mheshimiwa Sayyid Sistani”.
Kanali Othmani Ghanimiy mkuu wa vikosi vya Furaat Ausat alipo kutana na wapiganaji wa kujitolea wa kikosi cha Abbasi (a.s) alisema kua: “Hakika wapiganaji wa kikosi hiki wanahamasa kubwa zaidi ya matarajio, wanashiriki mazowezi kwa kujituma sana jambo ambalo linatia furaha na matumaini kwa wakazi wa Karbala tukufu na Iraq kwa Ujumla, bila shaka ushindi utapatikana haraka madam tunawapiganaji shujaa kama hawa, kikosi hiki kinatofautiana na vikosi vingine, kikosi hiki kimebeba jina la Abbasi (a.s) hilo jambo la kwanza, jambo la pili kimeanzishwa katika mji ambao ni kiini cha mapinduzi dhidi ya dhulma na matwaghuti, mambo hayo yanawafanya wapiganaji wa kikosi hiki wahisi jukumu kubwa mbele yao, wapiganaji wake wanauwezo mkubwa wa kubeba jukumu hilo”.
Kumbuka kua kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji Liwaau ya 26/ Hashdi Sha’abi kilishiriki katika vita nyingi za kukomboa ardhi ya Iraq kutoka katika udhibiti wa magaidi wa Daesh, na kilipewa majukumu ya kupigana ambayo kiliweza kuonyesha ushujaa na uwezo wake kivita, pamoja na kutegemea imani ya kiongozi wa jeshi la Imamu Hussein Abulfadhil Abbasi (a.s), na wametoa mashahidi na majeruhi wengi katika vita hiyo.