Miongoni mwa misaada ya kibinaadamu: Hospitali ya rufaa Alkafeel yaendesha zowezi la kujitolea damu.

Maoni katika picha
Kufuatia kuingia siku ya kimataifa ya kujitolea damu, hospitali ya rufaa Alkafeel chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu kwa kushirikiana na ofisi ya afya ya mkoa wa Karbala/ benki ya damu, inaendesha zowezi la kujitolea damu ambalo idadi kubwa ya wananchi na watumishi wake wameshiriki kutoa damu, kwa lengo la kuchangia damu kwa ajili ya wagonjwa wanao takiwa kuongezwa damu, na wametoa ujumbe kua mahitaji ya damu ni endelevu, uwepo wa damu ya kutosha husaidia kuokoa maisha wa watu wengi.

Viongozi wa hospitali wamesema kua zowezi hili linasaidia kupata hakiba ya damu ya kutosha, hasa aina za damu adimu, kwa sababu ni muhimu sana kuwa na damu salamua za aina tofauti.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: