Atabatu Abbasiyya tukufu yampa zawadi mshindi wa shindano la mapambo mazuri na bora ya msahafu.

Maoni katika picha
Makamo katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu Mhandisi Abbasi Mussawi Ahmadi amemkabidhi zawadi mshindi wa kwanza katika shindano la mapambo bora na mazuri zaidi ya msahafu, lililo endeshwa siku za nyuma na kituo cha maarifa ya Quráni kuifasiri na kuichapisha chini ya Maahadi ya Quráni katika kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu ambacho ni miongoni mwa vitengo vya Atabatu Abbasiyya tukufu.

Mshindi wa kwanza ni Ustadh Muhammad Faalih Kaatwii, kazi yake imezishinda kazi zote zilizo wasilishwa katika kamati ya majaji, na kuifanya kupata nafasi ya kwanza.

Hafla ya kukabidhi zawadi imehudhuriwa na mkuu wa kituo cha maarifa ya Quráni kuifasiri na kuichapisha Mheshimiwa Shekh Dhiyaau-Dini Zubaidi, ambaye ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Baada ya kuchapishwa Quráni tukufu kwa mara ya kwanza kuchapishwa na raia halisi wa Iraq, imekua ni muhimu kupata mapambo mapya na mazuri, ndio tukafanya mashindano haya ili tumeze kuchagua mapambo bora na mazuri zaidi kwa ajili ya kuyatumia katika nakala mpya itakayo chapishwa”.

Akaongeza kua: “Leo tunatoa zawadi kwa mbunifu na mshindi wa mapambo Ustadh Muhammad Faalih Kaatwii kutoka mkoa wa Dhiqaar kwa kumpa shahada na zawadi ya pesa kwa kazi nzuri aliyo fanya ya kutengeneza mapambo mazuri yanayo pendeza katika msahafu, zawadi hii ni sehemu ya kumshajihisha na kuthamini kazi yake”.

Naye mshindi wa nafasi ya kwanza Ustadh Muhammad Faalih Kaatwii akasema kua: “Tumeshiriki katika shindano hili kwa Baraka za Abulfadhil Abbasi (a.s), namshukuru Mwenyezi Mungu nimepata nafasi ya kwanza na hatimae nimepewa zawadi ndani ya eneo hili takatifu, jambo kubwa zaidi kwangu ni kupata nafasi ya kukitumikia kitabu cha Mwenyezi Mungu mtukufu, huenda kazi hii inaweza kunipa shifaa katika siku ambayo haitamfaa mja mali wala watoto”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: