Wanashiriki katika matukio ya kidini kama walivyo shiriki katika vita: Kikosi cha Abbasi (a.s) chafanya hafla ya kuwapongeza wapiganaji wake walioshiriki katika masomo ya Dini.

Maoni katika picha
Uongozi wa kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji (Liwaau/26 ya Hashdi Shaábi) umefanya hafla ya kuwapongeza wapiganaji wake waliopata nafasi za juu katika mitihani ya kufunga mafunzo ya Dini yaliyo tolewa na kitengo cha maelekezo ya kidini cha kikosi hicho, hafla imefanywa ndani ya ukumbi wa ofisi za kikosi hicho katika mkoa wa Karbala na kuhudhuriwa na kiongozi mkuu wa kikosi Shekh Maitham Zaidi na jopo la viongozi na wapiganaji.

Shekh Maitham Zaidi amesema kua: “Hakika masomo ya Dini ni muhimu sana kwa ajili ya kuwajenga wapiganaji walio itikia fatwa ya jihadi”, akasisitiza kua: “Hatuwalazimishi waumini wa Dini au madhehebu zingine kufuata Dini au dhehebu Fulani, kubwa tunalo hitaji ni kumfanya mpiganaji awe mzalendo wa taifa na raia wake, awe mwenye kuwapenda watu wa tabaka zote katika jamii, huo ndio msingi mkubwa wa kibinaadamu unao hubiriwa na Dini zote kwa ajili ya maendeleo ya taifa letu kipenzi”.

Mkuu wa kitengo cha maelekezo ya kidini katika kikosi cha Abbasi Shekh Qassim Aljaburi amesema kua: “Semina hii imefanywa kutokana na maelekezo ya kiongozi mkuu wa kikosi cha Abbasi, wakufunzi wamekwenda kufundisha vikosi mbalimbali katika maeneo tofauti hapa mchini, kuna zaidi ya wapiganaji (100) waliopata alama za juu kwa wastani wa asilimia (97) na zaidi katika masomo yao, utowaji wa zawadi unaonyesha umuhimu wa semina hizo”, Akasema: “Semina hizi zinaumuhimu mkubwa sana baada ya kumaliza vita kwani zinawajenga wapiganaji kua watu wema katika jamii”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: