Tawi la Maahadi ya Quráni katika mkoa wa Baabil lapokea zaidi ya washiriki (5000) wa semina za kiangazi.

Maoni katika picha
Maadi ya Quráni tukufu tawi la Baabil chini ya Atabatu Abbasiyya imepokea wanafunzi watakao shiriki katika semina za Quráni za majira ya joto (kiangazi), imepokea zaidi ya wanafunzi (5000) ambao imewaweka kwenye Misikiti na Husseiniyya za Baabil.

Wanasemina wanafundishwa Quráni, Aqida, Fiqhi, pamoja na Akhlaqi na Sira ya watu wa nyumba ya Mtume (a.s), chini ya wakufunzi walio bobea tena kwa kufuata ufundishaji wa kisasa, yanafundishwa masomo tofauti chini ya anuani moja isemayo (mwenendo wa mwanafunzi mwema), hii ni juhudi ya Atabatu Abbasiyya tukufu kuhakikisha wanafunzi wanatumia vizuri kipindi cha likizo za kiangazi.

Mkuu wa Maahadi ya Quráni tukufu Shekh Jawadi Nasrawi ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Idadi ya washiriki wa semina hizi imekua inaongezeka mwaka baada ya mwaka, mwaka huu kuna ongezeko kubwa katika kila mkoa tuliko weka semina”.

Akaongeza kua: “Mafanikio ya semina hizi yanatokana na wazazi kuona umuhimu wake kwani watoto wao hufundishwa Quráni, sira na masomo ya Aqidq na Akhlaqi”.

Akasisitiza kua: “Tumeandaa kila kinacho hitajika kwa mwanafunzi ikiwa ni pamoja na usafiri wa kwenda na kurudi pia kuna zawadi za wale waatakao fanya vizuri katika mambo mbalimbali ya kimasomo”.

Tambua kua semina za Quráni ni moja ya harakati muhimu ya Maahadi ya Quráni tukufu chini ya Atabatu Abbasiyya, tunatarajia kutengeneza kizazi kinacho fuata mafundisho ya Quráni na mwenendo wa Mtume na watu wa nyumbani kwake (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: