Atabatu Abbasiyya tukufu yaadhimisha fatwa tukufu iliyo nusuru Iraq ikiwa ni awamu ya nne ya kongamano la fatwa tukufu ya kujilinda

Maoni katika picha
Chini ya kauli mbiu isemayo: (Nyie ni fahari na utukufu wetu mnapongezwa na kila umma) kuadhimisha kumbukumbu ya fatwa ya Marjaa Dini mkuu ya kuilinda Iraq na maeneo matukufu, na kuadhimisha ushindi mkubwa uliopatikana dhidi ya magaidi wa Daesh kwa kukomboa maeneo yote waliyokua wameyateka hapa Iraq, Atabatu Abbasiyya tukufu imefanya kongamano la nne la kuadhimisha fatwa tukufu ya kujilinda kuanzia (23 hadi 24 Shawwal 1440h) sawa na (27 hadi 28 Juni 2019m) ndani ya ukumbi wa Imamu Hassan (a.s).

Hafla ya ufunguzi wa kongamano hilo imepata mahudhurio makubwa ya viongozi wa wawakilishi wa vikundi tofauti, ikiwa ni pamoja na kuhudhuriwa na kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu na katibu wake mkuu pamoja na jopo la viongozi wa juu, na wawakilishi wa Ataba na mazaru takatifu.

Baada ya kusomwa Quráni ya ufunguzi pamoja na surat Fat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi wa Iraq, ukaimbwa wimbo wa taifa na wimbo wa Atabatu Abbasiyya tukufu (Lahnul-Iba), halafu ukafuata ujumbe wa kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi.

Baada yake mshairi bwana Ali Swaffaar akaburudisha masikio ya wahudhuriaji kwa kusoma kaswida ya kimashairi kuhusu fatwa tukufu ya kujilinda na namna ilivyo itikiwa, kisha ukafuata ujumbe wa kamati ya kongamano la Spaika ulio wasilishwa na Shekh Abbasi Quraishi, akawaomba wanao husika kukabidhi miili ya mashahidi kwa familia zao na kuwaadhibu wote walio husika na mauwaji hayo kwa mujibu wa sheria.

Kisha ukatangazwa uzinduzi wa kitabu kikubwa (kuhusu fatwa ya kujilinda), tangazo lilitolewa na makamo rais wa kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya na mtendaji mkuu wa mradi wa uwandishi wa kitabu hicho Ustadh Ahmadi Swadiq.

Hafla hiyo ilipambwa na maonyesho ya filamu mbili, ya kwanza ilikua na anuani isemayo: (Jambo kubwa lililozuwia kimbunga cha simba), na filamu ya pili ilikua na anuani isemayo: (Historia tukufu ya majemedari wa Iraq).

Baada ya hapo washiriki wakaelekea katika uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu kwenye uzinduzi wa maonyesho ya picha za aina mbalimbali kuhusu fatwa ya kujilinda na namna ilivyo itikiwa pamoja na yaliyo tokea kutokana na fatwa hiyo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: