Vipengele muhimu alivyo ongea Marjaa Dini mtuu katika khutuba ya swala ya Ijumaa

Maoni katika picha
Marjaa Dini mkuu kwenye khutuba ya pili ya swala ya Ijumaa iliyo swaliwa ndani ya ukumbi wa haram ya Imamu Hussein (a.s) tarehe (24 Shawwaal 1440h) sawa na (28 Juni 2019m), chini ya uimamu wa Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi amezungumza vipengele vingi vya kimaadili na kimalezi vinavyo endana na hali halisi ya maisha ya sasa, miongoni mwa vipengele muhimu alivyo ongea ni:

 • - Umma hujifaharisha kwa utamaduni wake, tamaduni hutofautiana kadri umma utakavyo kua na malezi mazuri ndio utakavyo kua na utamaduni bora.
 • - Utamaduni wa malezi mema ni muhimu zaidi kwetu.
 • - Kuna aina za tamaduni ambazo hutambulisha umma.
 • - Kitabu ni sehemu ya vitu vinavyo unda utamaduni.
 • - Tunahitaji kua na misingi imara ya kijamii.
 • - Kila mtu anatakiwa kuchunga muda na umri wake autumie katika mambo yenye faida.
 • - Umri ni mfupi hautoshi kukamilisha mataraio yetu yote.
 • - Leo tuna tatizo linguine kubwa kabla ya tatizo la makuzi, nalo ni tatizo la watoto wadogo kujishughulisha zaidi na vifaa vya kisasa.
 • - Mtu mwenye Dini anatakiwa kua na mbleki, Myenyezi Mungu anasema (Wasimamishe hakika wanaulizwa).
 • - Hata kama hauna Dini kua na ubinadamu, kwa nini ufuate njia mbaya katika kuamiliana na watu?
 • - Taifa linahitaji watu wenye utamaduni mzuri.
 • - Yatupasa kua makini kwa watoto wetu, tufuatilie matumizi yao ya mitandao ya mawasiliano ya kijamii.
 • - Familia inatakuwa kumrekebisha mototo na sio kulalamika bila kuchukua hatua za kumrekebisha.
 • - Matumizi ya mitandao ya kijamii yamekua na athari kubwa, kuna baadhi ya watu wanakesha katika mitandao hadi wanachelewa kwenda kazini na wanakua wavivu kazini.
 • - Mtu anatakiwa kuongea maneno mazuri yenye faida kwa watu wala sio yenye madhara kwa watu.
 • - Thamani ya mtu huonekana katika maneno na maandishi yake, ni muhimu sana kuchunga maneno yako unapo ongea na kuandika.
 • - Utamaduni wa matusi umeenea sana, wala sio utamaduni wetu, taifa hili linajulikana kua lina watu wenye utamaduni mzuri, wenye adabu na akili pevu.
 • - Vijana wanaweza kuacha utamaduni wetu kutokana na wazazi, mwalimu na rafiki kuacha majukumu yao.
 • - Sidhani kama kuna mtu anaridhika taifa letu kua na utamaduni mbaya, utamaduni wa matusi, shutma na maneno machafu.
 • - Taifa limejaa watu wenye moyo wa kujitolea lazima liwe na utamaduni unao endana na watu hao.
 • - Tusiwape nafasi watoto wetu ya kufanya watakavyo.
 • - Mwenye kutukana hua mtu duni, tulinde ndimi zetu na matusi.
 • - Hili ni jukumu la kila mtu katika jamii, wala haliwezi kuongelewa na kuisha kwa khutuba moja wala mia moja, zinahitajika juhudi za jamii nzima.
 • - Familia inawajibika kwa watoto wake, isiruhusu tamaduni mbaya, Iraq ni taifa la watu wenye tamaduni nzuri walioshinda mitihani mingi pamoja na fitna ya Daesh, mzazi anatakiwa aongee na mwanae ili ajue uwelewa na akili yake na hili ni jukumu la kila mtu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: