Kama kawaida katika kuomboleza misiba ya watu wa nyumba ya Mtume (a.s), Atabatu Abbasiyya imeandaa ratiba maalum ya maombolezo yenye vipengele vingi, pamoja na ushiriki wake katika kuwahudumia mazuwaru, ratiba hiyo inavipengele vifuatavyo:
- 1- Kupokea mawakibu za waombolezaji kupitia kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu.
- 2- Mgahawa (mudhifu) wa Abulfadhil Abbasi (a.s) umeandaa mamia ya sahani za chakula na kukigawa kwa mazuwaru kupitia madirisha ya nje.
- 3- Kuweka vikao vya mihadhara (majlisi) ndani ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s).
- 4- Kuweka majlisi maalum kwa ajili ya watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) katika ukumbi wa utawala.
- 5- Kufanya matembezi ya kuomboleza kwa watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa ajili ya kumpa pole bwana wa mashahidi Abu Abdillahi Hussein (a.s).
Fahamu kua Atabatu Abbasiyya huandaa ratiba maalum katika kila tukio linalo husu watu wa nyumba ya Mtume (a.s).