Waombolezaji wa kifo cha Imamu Swadiq (a.s): Mamia ya sahani za chakula zatolewa na Atabatu Abbasiyya kwa waombolezaji

Maoni katika picha
Mgahawa (mudhifu) wa Abulfadhil Abbasi kupitia ratiba iliyo jiwekea katika kuomboleza kifo cha Imamu Jafari (a.s), umegawa mamia ya sahani za chakula kwa mazuwaru na waombolezaji waliokuja kumpa pole Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s).

Wamegawa chakula kupitia madirisha maalum yaliyo pangwa na kitengo cha mgahawa (mudhifu) yaliyopo sehemu zenye msongamano mkubwa wa mazuwaru, ugawaji wa chakula unafanyika haraka haraka bila kusababisha foleni wala kutatiza harakati za mazuwaru.

Fahamu kua katika ziara zinazo hudhuriwa na watu wengi mgahawa hugawa chakula kwa watu kusimama kwenye mstari, huwa kuna mstari wa wanaume na wa wanawake, watumishi huhakikisha kila mmoja anapata chakula, hii ni kutokana na uzowefu waliopata kwa miaka mingi katika shughuli za kugawa chakula, watumishi wa mgahawa wa mwezi wa bani Hashim (a.s) wanajulikana kwa kutoa huduma nzuri kwa mazuwaru na mpangilio mzuri walio nao.

Sio katika mji wa Karbala peke yake bali kila mahala wanapo kwenda kuhudumia mazuwaru, fahamu kua makundi makubwa ya waumini –mmoja mmoja na mawakibu/ vikundi- kutoka ndani na nje ya Karbala wanakuja kumpa pole Abu Abdillahi Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) kutokana na kifo cha Imamu Swadiq (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: