Katika kuendeleza mafanikio yake: Mradi wa (Kiongozi wa wasomaji wa taifa) inaanza awamu ya tano ukiwa na zaidi ya wanafunzi (120)

Maoni katika picha
Kwa ushiriki wa zaidi ya wanafunzi (120) kutoka mikoa tofauti ya Iraq, Jumatatu (27 Shawwal 1440h) sawa na (1 Julai 2019m) tumeanza kutekeleza ratiba ya awamu ya tano ya mradi wa kiongozi wa wasomaji wa kitaifa, unao simamiwa na kituo cha wasomaji na mahafidh chini ya Maahadi ya Quráni tukufu katika Atabatu Abbasiyya ndani ya jengo la Alqami.

Ratiba ya siku ya kwanza ilijikita katika kupokea wanafunzi na kuwaingiza katika orodha maalum pamoja na kuwapanga katika madarasa, ratiba ya mradi huu itadumumu miezi miwili, watasoma kwa wingi Quráni, Aqida na Fiqhi pamoja na namna anavyotakiwa kuwa msomaji wa Quráni tukufu, pia kutakua na nadwa, mihadhara na mahafali za kidini.

Zitafundishwa madrasa tano za usomaji: (Madrasa ya Haafidh Khaliil Ismaili kwa mahadhi ya kiiraq, Madrasa ya Shekh Abdulfataah Shaáshaai, Madrasa ya Shekh Muhammad Swidiiq Minshawi, Madrasa ya Sheik Shahata Muhammad Anuur na Madrasa ya Shekh Abu Ainaini Shaishai), pia kuna idara maalumu ya watoto wa mashahidi na mujahidina katika Hashdi Shaábi ambao ni wanafunzi wapya.

Fahamu kua mradi huu unaendeshwa na walibu wenye uwezo mkubwa, unalenga kutengeneza kizazi cha wasomi wa Quráni wenye uwezo mkubwa kupitia kulea vipaji vya watoto katika usomaji wa Quráni ndani ya muda mfupi, unawalenga watoto wa shule za msingi na sekondari kutoka mikoa tofauti ya Iraq, na kutumia vizuri msimu wa likizo za kiangazi (majira ya joto), kitindi hiki cha miezi miwili takriban hutumiwa kama sehemu ya kwanza ya mradi huu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: