Kitengo cha Dini kinapambana na mambo yasiyokua na ushahidi wa kisheria yaliyo zushwa na wajinga

Maoni katika picha
Kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya kimekua kikitoa machapishe ya ukubwa torauti, vijibabu, vitabu na majarida yenye maudhui za Fiqhi, Aqida, Akhlaq na mambo ya kijamii, yenye lugha rahisi inayo eleweka na kila mtu, huku kila kitu kikiwekewa ushahidi wa aya na hadithi za Mtume (s.a.w.w) pamoja na za Maimamu wa Ahlulbait (a.s).

Miongoni mwa machapisho hayo ni kitabu cha: (Mambo ya ajabu yasiyokua na ushahidi wa kisheria yanayotokana na uzushi wa wajinga), kimeandika mambo yasiyokua na dalili za kisheria, yameelezewa na kubainisha upotovu wake pamoja na kutahadharisha watu na mambo hayo.

Kutokana na kukubalika kwa kitabu hicho tayali kimesha chapishwa mara kadhaa, hadi sasa kinapatikana katika kituo vya mauzo ya moja kwa moja kilicho chini ya kitengo cha Dini mkabala na mlango wa Imamu Hassan (a.s) katika Atabatu Abbasiyya tukufu, pia unaweza kukipakua kutoka katika toghuti ya kitengo cha Dini kupitia linki ifuatayo: https://alkafeel.net/religious/index.php?iss
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: