Shekh Swalahu Karbalai asisitiza umuhimu wa kuzisaidia taasisi za kibinabamu

Maoni katika picha
Shekh Swalahu Karbalai Rais wa kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya tukufu amesisitiza umuhimu wa kuzisaidia taasisi za kibinadamu, zinazo toa huduma muhimu ambazo hata baadhi ya taasisi za serikali zimeshindwa kutoa, hasa taasisi zinazo saidia mayatima.

Ameyasema hayo katika ujumbe aliotoa kwenye hafla iliyo andaliwa na taasisi ya Nurul-Hussein (a.s) inayo lea mayatima katika mkoa mtukufu wa Karbala, hafla hiyo ilikua ya kuwazawadia vijana ambao ni mayatima vyombo vya ndani kwa ajili ya ndoa.

Shekh Swalahu amesifu kazi kubwa inayo fanywa na taasisi hiyo ya kutunza na kulea mayatima, na kuwapa misaada mbalimbali, akawatakia mafanikio mema katika kazi zao.

Kumbuka kua hafla hii imefanywa katika eneo la Mubarra Shami ndani ya mji wa Karbala, na kuhudhuriwa na viongozi tofauti wa Dini pamoja na viongozi mbalimbali wa makundi ya wanawake na makundi ya kijamii.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: