Ndani ya malalo ya mwanae: Wapenzi wa Ummul Banina wanaadhimisha kuolewa kwake na kiongozi wa waumini (a.s)

Maoni katika picha
Wanahistoria walio andika kuhusu Abulfadhil Abbasi (a.s) wametofautiana tarehe ya ndoa ya Imamu Ali na Ummul Banina (a.s), pamoja na kutofautiana huko sio sababu ya kuacha kufanya utafiti wa swala hilo la kihistoria, jambo hilo limewasukuma wapenzi wa Ummul Banina (a.s) kufanya utafiti na kugundua tarehe ya ndoa hiyo tukufu kua ni (2 Dhulqaada), imeanza kuadhimishwa siku hiyo ndani ya malalo ya mwanae Abulfadhil Abbasi (a.s) chini ya usimamizi wa watumishi wa Ataba hiyo takatifu.

Maadhimisho hayo yamepewa jina la (Hafla ya kongamano la kwanza la kuadhimisha kuolewa kwa Ummul Banina (a.s) na Imamu Ali –a.s-) hafla hiyo imefanyika ndani ya ukumbi wa Imamu Hassan (a.s) katika Atabatu Abbasiyya tukufu, ilifunguliwa kwa Quráni tukufu iliyo somwa na bwana Mustwafa Swarraaf msomaji wa Ataba mbili takatifu.

Ukafuata ujumbe kutoka kwa wasimamizi wa kongamano hilo, ulio wasilishwa na Ustadh Saádi Ali Hussein kutoka kikundi cha Nurul-Hussein (a.s), aliye bainisha namna walivyo weza kugundua tarehe ya kumbukumbu hii na njia walizo tumia kuhesabu muda kuanzia tarehe ya kuzaliwa kwa Abulfadhil Abbasi (a.s) kurudi nyuma, akazunguma kuhusu utukufu wa Ummul Banina (a.s), na namna alivyo fanywa kua miongoni mwa milango ya Mwenyezi Mungu ya kukidhi haja za waumini.

Kisha zikafuata kaswida na mashairi kutoka kwa washairi wafuatao:

  • - Ridhwa Khafaji.
  • - Muhammad Fatwimi.
  • - Auda Dhwahi.
  • - Hussein Akili.
  • - Haidari Mwalimu
  • - Faiz Miyali
  • - Imaad Issawi
  • - Dhwiyau Badri.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: