Jumuwiya ya Skaut ya Alkafeel inaendelea na ratiba ya masomo ya awamu ya tatu

Maoni katika picha
Jumuwiya ya Skaut ya Alkafeel chini ya idara ya watoto na makuzi katika Atabatu Abbasiyya tukufu inaendelea kutoa mafunzo katika ratiba ya awamu ya tatu, ikiwa na washiriki zaidi ya (400), miongoni mwa masomo wanayo fundishwa ni yale ya Akhlaq yenye anuani isemayo: (Akhlaq za kijamii) ambapo wanafundishwa mambo mbalimbali ya ki-akhlaq katika Skaut, kama vile kutoa salamu na kuheshimu watu.

Kipengele cha pili kinahusu vipaji na ufundi, kinahusisha masomo ya kanuni za msingi katika uchoraji na tabaka za sauti katika uwimbaji pamoja na tajwidi katika usomaji wa Quráni sambamba na mihadhara kuhusu kanuni za uandishi wa habari, lengo ni kuwafanya vijana wa Skaut wajue kila kitu chenye umuhimu pamoja na kutumia vizuri uwezo walio nao.

Upande wa michezo pia umepewa umuhimu mkubwa sawa na vitu vingine, imeandaliwa ratiba ya michezo ya aina mbalimbali kwa wanaskaut, pia kunaratiba ya kutembelea bustani ya Imamu Hussein (a.s), kikihitimishwa na mchezo wa igizo pamoja na mashindano ya mambo ya kutumia akili.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: