Watumishi wa kitengo cha uangalizi wa haram tukufu wanafanya kazi ya kuosha kubba la malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s)

Maoni katika picha
Watumishi wa kitengo cha uangalizi wa haram tukufu ya Atabatu Abbasiyya wameanza kazi ya kuosha kubba ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kwa ajili ya kuhifadhi uimara wake na muono wake jambo linalo saidia kuendelea kuwa imara na kutoharibiwa na mabadiliko ya hewa, kazi hii itahitimishwa kwa kuosha minara miwili.

Tumeongea na rais wa kitengo hicho bwana Nizaar Ghina Khaliil kuhusu kazi hiyo amesema kua: “Watumishi wa kitengo chetu huosha kubba kila baada ya muda Fulani, kwa ajili ya kudumisha usafi wa kubba tukufu na muonekano wake pamoja na kuilinda isiharibiwe na mabadiliko ya hali ya hewa”.

Akaongeza kua: “Kazi ya kusafisha hugawanywa katika hatua tofauti, hutumika vifaa maalum vya usafi katika kazi hiyo, visivyo kua na athari yeyote kwenye vifuniko vya dhahabu vilivyopo katika kubba hiyo, hutumika kitambaa cha kotoni kukaushia vifuniko vya dhahabu baada ya kuoshwa”.

Akasema: “Kesho tunatarajia kumaliza kazi ya kuosha kubba tukufu la mwezi wa bani Hashim (a.s) kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu, kisha tutaanza kuosha minara miwili”.

Fahamu kua kitengo cha uangalizi wa haram tukufu kina majukumu mengi ndani ya haram tukufu ya Abbasi (a.s) kama vile kazi za usafi na kutandika mazulia nazinginezo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: