Kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji kimetangaza matokeo ya siku ya kuanza misafara ya mahujaji wa nyumba tukufu ya Mwenyezi Mungu

Maoni katika picha
Kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji (Liwaa/26 Hashdi Shaábi) kimetangaza kua jumla ya misafara (79) ikiwa na mahujaji wasiopungua (1783) kutoka mikoa tofauti ya Iraq imeondoka kwenda katika nyumba tukufu ya Mwenyezi Mungu kutekeleza faradhi ya Hija.

Wamesema kua katika siku ya kwanza jumla ya misafara (61) imewasili katika mji wa Karbala ikiwa na mahujaji wasiopungua (1411) kutoka mikoa ya Waasit, Diyala, Muthanna na Diwaniyya, huku misafara mingine (18) kutoka Anmbaar kupitia barabara ya (160) hadi wilaya ya Nakhibu ikiwa na mahujaji wasiopungua (372) ikiwasili pia.

Kumbuka kua kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji kilikua kimesha tangaza kutekeleza wajibu kiliopewa na jeshi la serikali, wa kuimarisha usalama katika barabara inayo tumiwa na mahujaji wa nyumba tukufu ya Mwenyezi Mungu katika eneo lenye umbali wa zaidi ya (km 200) sehemu ya Urúr mpakani katika kutekeleza wajibu wake wa kiulinzi na kiutumishi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: