Asisitiza kua makumbusho ya Alkafeel inahaki zaidi kuliko mahala popote… Mkazi wa Bagdad aipa makumbusho ya Alkafeel vifaa kale adim

Maoni katika picha
Idara ya makumbusho ya Alkafeel katika Atabatu Abbasiyya tukufu imeripoti kupokea vifaa kale adim kutoka kwa Sayyid Karim Abdulhussein mkazi wa Bagdad.

Kwa mujibu wa maelezo ya rais wa kitengo Ustadh Swadiq Laazim: “Leo makumbusho ya Alkafeel imepokea zawadi ya vifaa kale adim, vifaa hivyo ni: (Sarafu adim zinazo nasibishwa na zama za Imamu Ridhwa –a.s- pamoja na sarafu zingine za fedha za aina mbalimbali, sanduku moja kubwa na lingine dogo na vyombo viwili vyenye mishikio iliyo wekwa mapambo na vinginevyo) jina lake limeingizwa katika orodha ya watu waliozawadia Atabatu Abbasiyya tukufu”.

Akasema: “Makumbusho inavifaa kale vya aina tofauti, asilimia kubwa tumepewa zawadi baada ya kufungua milango ya kupokea zawadi kutoka kwa waumini, pia ni ishara ya kuonyesha utukufu wa Abulfadhil Abbasi (a.s)”.

Sayyid Karim Abdulhussein amefurahi sana baada ya kufanikiwa kutoa zawadi hizo, amesema kua anahisi amani katika nafsi yake baada ya jina lake kuandikwa katika makumbusho ya Abulfadhil Abbasi (a.s), akasisitiza kua makumbusho ya Alkafeel inahaki zaidi ya kupewa vifaa kale hivyo kushinda mahala pengine popote.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: