(Kuwapa maji ya kunywa mahujaji ni utukufu kwetu) ni kauli mbiu inayotumiwa na watumishi wa idara ya maji katika kuwapa maji mahujaji wa nyumba tukufu ya Mwenyezi Mungu

Maoni katika picha
(Kuwapa maji mahujaji ni utukufu kwetu) ni kauli mbiu inayo tumiwa na watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) katika kuwapa maji mahujaji wa nyumba tukufu ya Mwenyezi Mungu, tangu ilipo anza kuongoka misafara ya mahujaji kwenda kutekeleza ibada ya hija kwa kutumia njia ya barabara (Nakhiib – Arúr), Atabatu Abbasiyya tukufu imekua ikifanya baadhi ya mambo, kama kugawa maji na mamia ya barafu kupitia vituo vya (RO) vinavyo tumika kuhifadhi maelfu ya lita za maji kwa kushirikiana na kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji chenye jukumu la kulinda usalama wa barabara inayo tumiwa na mahujaji.

Kiongozi wa idara ya maji bwana Ahmadi Hanun ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Baada ya kupewa jukumu na uongozi wa Atabatu Abbasiyya tukufu la kuwahudumia wageni wa Mwenyezi Mungu, tumeandaa mkakati maalum wa kutekeleza jukumu hilo ambalo ni fahari kwetu sambamba na kuwahudumia mazuwaru wa Abulfadhil Abbasi (a.s), kwa sababu kiongozi wetu Abulfadhil Abbasi (a.s) alikua mnyweshaji wa maji, nasisi tunawapa maji ya kunywa mahujaji, tumeanza kutoa huduma ya kugawa maji tangu msafara wa kwanza wa mahujaji, tena utawakuta watumishi wa kitengo hiki wanashindana katika kutoa huduma”.

Akaongeza kua: Maji huchukuliwa kila siku kutoka kituo cha Atabatu Abbasiyya tukufu cha (RO) ambacho pia wanatumia mazuwaru wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), huwekwa katika magari maalum kwa kiwango kinacho hitajika halafu huchukuliwa na barafu kutoka katika kiwanda cha kutengeneza barafu kilicho chini ya Atabatu Abbasiyya kwa ajili ya kuwapa maji ya baridi, maji hayo yamewekwa katika deli zaidi ya (90) zilizopo kwenye maeneo ya kupumzikia mahujaji pamoja na kwenye deli zilizopo sehemu za ukaguzi wa paspoti”.

Mahujaji wameshukuru sana kupewa huduma hii na Atabatu Abbasiyya tukufu, sambamba na huduma zingine nyingi wanazo pewa na Ataba tukufu ikiwa ni pamoja na kuimarisha ulinzi katika barabara zinazo tumiwa na mahujaji kwenda katika nyumba tukufu ya Mwenyezi Mungu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: