Kitengo cha utalii wa kidini katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimetenga gari (15) kwa ajili ya kubeba wageni wa Mwenyezi Mungu kuwapeleka katika nyumba takatifu

Maoni katika picha
Kwa maelekezo ya uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu na kwa kushirikiana na kamati kuu ya Hija na Umra, pia kutokana na ratiba maalum ya kipindi cha Hija, kitengo cha utalii wa kidini katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimeshiriki kubeba mahujaji wa nyumba ya Mwenyezi Mungu wa mwaka (1440h) kuwapeleka katika nyumba takatifu kutoka mikoa tofauti ya Iraq, kwa kutenga gari (15) za kitalii.

Haya yamesemwa na rais wa kitengo cha utalii wa kidini katika Atabatu Abbasiyya tukufu Mhandisi Jafari Saidi Jafari kwa mtandao wa kimataifa Alkafeel: “Kitengo chetu kimepata heshima ya kubeba wageni wa Mwenyezi Mungu, kwa kutumia gari (15) za kitalii, tunawachukua kutoka kwenye miji yao hadi katika nyumba takatifu ya Maka na Madina”.

Akaongeza kua: “Gari zetu zimechukua mahujaji kutoka mikoa tofauti na kuwapeleka Maka na Madina kupitia mpaka wa Urúr, kisha yatawarudisha katika nchi yao kipenzi baada ya kumaliza ibada ya Hija Insha-Allah”.

Fahamu kua kitengo cha utalii wa kidini katika Atabatu Abbasiyya tukufu husafirisha waumini kipindi chote cha mwaka kwa kuwapeleka maeneo matakatifu Iran na Sirya pamoja na safari za ibada ya Umra, chini ya usimamizi wa wasomi wa Dini na viongozi wa idara wenye uzowefu mkubwa walio pata kutokana na kushiriki kwao katika misafara hoyo kwa miaka mingi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: