Maoni katika picha
Idara hii inatunza miswala kielimu na kwa kufuata kanuni za makumbusho katika utunzaji, kazi hiyo hupita katika hatua kadhaa, miongoni mwa hatua hizo ni:
- 1- Kuandaa ukurasa wa maelezo (ukubwa na aina).
- 2- Kuondoa vumbi kwenye mswala.
- 3- Kuweka alama maalum kwenye kila mswala inaitwa (Barkod).
- 4- Kutumia baadhi ya vitu vya asili kwa ajili ya kufukuza wadudu na nge.
- 5- Mswala huvingirishwa kwenye bomba baada ya kuwekwa kwenye nailoni.
- 6- Mswala ufunikwa kwa kipande cha katani.
Fahamu kua makumbusho ya vifaa na nakala kale Alkafeel ni makumbusho ya kwanza kufunguliwa katika Ataba tukufu za Iraq, ilifunguliwa mwaka (2009) katika kumbukumbu ya kuzaliwa kwa bibi Zainabu (a.s), inaidadi kubwa ya vifaa kale vyenye karne na karne.