Kituo cha kuosha mazulia na makapeti katika Atabatu Abbasiyya tukufu kinafanya kazi kubwa ya kuosha mazulia

Maoni katika picha
Idara ya uoshaji wa mazulia chini ya kitengo cha usimamizi wa haram tukufu ya Atabatu Abbasiyya imeanza kazi ya kuosha mazulia yaliyopo ndani ya haram ya Abbasiyya itakayo fanyika kwa muda wa siku kadhaa.

Kiongozi wa uoshaji wa mazulia Ustadh Maitham Swakhiil amesema kua: “Kazi ya kuosha mazulia huongezeka katika mwezi wa Muharam na Safar na baada ya miezi hiyo kwa ajili ya kuweka mazingira ya usafi kwa mazuwaru watukufu wanaokuja kufanya ibada ndani ya maeneo ya Ataba tukufu”.

Akaongeza kua: “Kutokana na kuongezeka kwa kazi ya kuosha mazulia imelazimika uongozi wa Ataba tukufu uongeze vifaa vya kisasa ili kukiwezesha kituo kuosha mazulia mengi zaidi, pia kuna mpango wa kujenga kituo kikubwa zaidi Insha-Allah”.

Ustadh Maitham akataja vifaa vilivyo ongezwa na namna ya utendaji wake akasema kua: “Hupokea mazulia yanayo takiwa kuoshwa kutoka katika vitengo vya Ataba hususan kitengo cha utumishi ambacho ndio kipo karibu zaidi na mazuwaru kwa kuandaa sehemu za kuswalia na ziara na ndio kinacho husika na mazulia yaliyopo katika eneo la mazuwaru na ndio kinacho tandika na kutandua mazulia hayo yanapo chafuka na kuyaleta kwetu kwa ajili ya kuyaosha”.

Akaongeza kua: “Hatua za uoshaji zinatofautiana kutokana na kutofautiana kwa aina ya zulia (kapeti) huanza kuondoa vumbi kisha hupelekwa katika eneo la kuoshea halafu hukaushwa na kuwekwa juani, huku mablanketi huoshwa moja kwa moja kwa kutumia mitambo na sabuni nzuri za kunikia”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: