Kituo cha turathi za Karbala chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu kimeongeza muda wa kupokea tafiti zitakazo wasilishwa katika kongamano lake la kwanza la kimataifa liitwalo (Turathi zetu ndio utambulisho wetu)

Maoni katika picha
Kwa ajili ya kuwapa nafasi wasomi na watafiti, kituo cha turathi za Karbala chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimeongeza muda wa kupokea tafiti zitakazo wasilishwa katika kongamano la kimataifa litakalo fanywa chini ya usimamizi wa Atabatu Abbasiyya tukufu chini ya kauli mbiu isemayo: (Turathi zetu ndio utamaduni wetu) litakalo kua na anuani isemayo: (Nafasi ya turathi za Karbala katika maktaba za kiislamu).

Kituo kimeongeza muda wa kupokea tafiti, kwani mwisho wa kupokea ulikua ni (7/ 8/ 2019m) sasa utakua (7/ 9/ 2019m).

Muda umeongezwa kwa ajili ya kutoa nafasi kwa wasomi na watafiti wengi zaidi wanaotaka kuwasilisha tafiti zao kwa mujibu wa kanuni zilizo tangazwa.

Fahamu kua kituo cha turathi za Karbala kilikua kimesha watangazia wasomi na watafiti nafasi za kuandaa mada zitakazo wasilishwa katika kongamano chini ya kauli mbiu isemayo: (Turathi zetu ndio utambulisho wetu) na anuani isemayo (Nafasi ya turathi za Karbala katika maktaba za kiislamu), linalo tarajiwa kufanyika tarehe (7-8 Novemba 2019m) sawa na (10-11 Rabiul Awwal 1441h), tafiti zinatarajiwa ziwe zinahusu turathi za Karbala.

Kwa ajili ya kuangalia mada na masharti ya kushiriki ingia katika link ifuatayo (https://alkafeel.net/news/index?id=8944) au wasiliana nasi kwa sim namba (009647729261327) namba hiyo pia inapatikana katika (Viber, Whatsapp na Telegram) au wasiliana nasi kwa barua pepe ifuatayo (turath@Alkafeel.net).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: