Katika kukamilisha ratiba yake, idara ya shule za Alkafeel za wasichana imefungua semina ya tatu ya (wabeba bendera) ambayo ni sehemu ya ratiba ya hema za Skaut za kiangazi awamu ya kumi inayo itwa (Mabinti wa Aqida), iliyo andaliwa kwa wasichana wanaosoma vyuo kutoka mikoa ya (Bagdad, Waasit, Qadisiyya na Diyala).
Kuhusu ratiba hii tumeongea na kiongozi wa idara ya shule za wasichana Alkafeel Ustadhat Bushra Alkinani amesema kua: “Lenge la kuweka masomo haya ni kutengeneza mazingira ya kuwasiliana kwa wanafuni baina yao, na kuongeza kiwango cha elimu zao pamoja na kuhakikisha wanatumia vizuri kipindi cha likizo za kiangazi kwa manufaa yao, ratiba hii ni muendelezo wa ratiba zingine za aina hii zilizo tangulia na muendelezo wa mafanikio yaliyo fikiwa, kutokana na mwitikio mzuri na kuongezeka kwa washiriki tumelazimika kuwagawa katika hema tofauti, ili tuweze kutoa fursa kwa washiriki wengi zaidi kwenye kila mkoa”.
Akafafanua kua: “Hema hizi zinakua na vipengele vingi, kuna vikpengele cha masomo ya utamaduni, familia na kiroho pamoja na kutembelea Ataba takatifu, pia kuna mihadhara ya Aqida na Akhlaq sambamba na kufundishwa namna ya kutoa huduma ya kwanza katika uokozi, na kuna kazi za mikono ambazo zinalenga kuibua vipaji, halafu kuna mashindano na michezo mbalimbali, pia kuna vikao vya usomaji wa Quráni na darasa mjadala ambalo huulizwa maswali na kujadiliwa mada mbalimbali”.
Kumbuka kua ratiba ya hema ni moja ya harakati za idara ya shule za wasichana Alkafeel iliyopo katika kituo cha Swidiqah Twahira (a.s), na ratiba yake hudumu ndani ya kipindi cha mwaka mzima, na hufundishwa mambo mbalimbali ya kielimu kwa ajili ya kujenga uwezo wa wanafunzi kielimu na kuibua vipaji vyao pamoja na kuwajenga kijamii, na hutolewa mihadhara mbalimbali ya kidini inayo wahimiza kupambana na mazingira halisi ya jamii.