Atabatu Abbasiyya tukufu imewekwa mapambo meusi kutokana na msiba wa kifo cha Imamu Baaqir (a.s)

Maoni katika picha
Kuta za Atabatu Abbasiyya tukufu na korido zake zimewekwa mapambo meusi kutokana na msiba wa kifo cha Imamu wa tano Muhammad Baaqir (a.s), yamewekwa mabango meusi yaliyo andikwa ujumbe unao ashiria msiba na huzuni waliyo nayo wafuasi na wapenzi wa Ahalulbait (a.s) kutokana na msiba huo.

Kama kawaida katika kuomboleza vifo vya watu wa nyumba ya Mtume (a.s) Atabatu Abbasiyya imeandaa ratiba kamili yenye vipengele vingi, kuna ufanyaji wa majlisi za kuomboleza ndani ya ukumbi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) sambamba na kufanya majlisi maalum kwa ajili ya watumishi wa Ataba ndani ya ukumbi wa utawala, kuna maandalizi ya kupokea waombolezaji mtu mmoja mmoja na mawakibu (vikundi), pamoja na kushiriki katika maukibu ya kuomboleza ya pamoja na watumishi wa bwana wa mashahidi na kwenda kumpa pole kwa kufiwa na mjukuu wake Imamu Baaqir (a.s).

Fahamu kua mwezi saba Dhulhijja ni siku aliyo kufa Imamu Muhammad bun Ali Albaaqir (a.s), nalo ni tukio linalo umiza nyoyo za wapenzi na wafuasi wa Ahlulbait (a.s) na huombolezwa siku hiyo kila sehem ya dunia.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: