Atabatu Abbasiyya tukufu yafadhili mafunzo ya mradi wa watoto katika chuo kikuu cha Baabil

Maoni katika picha
Katika ushirikiano wa Atabatu Abbasiyya tukufu na chuo kikuu cha Baabil, ugeni kutoka chuo hicho ukiongozwa na makamo rais wa chuo Dokta Qahtwaani Haadi Hussein, umetembelea Atabatu Abbasiyya tukufu na kukutana na kiongozi mkuu wa kisheria Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi.

Ugeni umeonyesha kufurahi na umetoa shukrani nyingi kwa Mheshimiwa kiongozi mkuu wa kisheria kutokana na misaada inayo tolewa na Ataba kwa vyuo vya Iraq kikiwepo chuo cha Baabil.

Tulipo ongea na makamo rais wa chuo hicho amesema kua: “Tumekutana na Mheshimiwa kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya, kikao chetu kimekua na faida kubwa kwa sababu tumezungumzia kuhusu kuwasaidia watu wasio kua na uwezo wowote katika jamii ambao ni tabaka la watoto”.

Akaongeza kua: “Tumeongelea mradi wetu unaohusiana na ratiba ya serikali, mradi wa kuanzisha kituo maalum cha watoto katika chuo kikuu cha Baabil, Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi ametupa habari njema kua Atabatu Abbasiyya itasaidia kwa kiasi kikubwa mradi huu, kwa kua mradi huu ni kwa faida ya jamii na unahusu watu muhimu katika jamii ambao ni tabaka la watoto”.

Akabainisha kua: “Watumishi wa mradi huo wanahitaji mafunzo ya hali ya juu na mafunzo hayo watapewa na watalamu wa Atabatu Abbasiyya, Mhueshimiwa ametuahidi kua watumishi wetu watafundishwa na watalamu wa Ataba tukufu”

Fahamu kua Atabatu Abbasiyya tukufu iliwahi kuendesha semina kuhusu tatizo la upweke wa watoto kwa walimu (30) wa chuo chini ya Dokta Shaamil Muhsin muwakilishi wa Atabatu Abbasiyya nchini Marekani.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: