Tambua wasifu muhimu wa dirisha hili lililotengenezwa kwa uhodari na umakini wa hali ya juu:
- - Lilisanifiwa na kuandaa mchoro wake na wachoraji bingwa waliotumia ufundi wao wote kuhakikisha linakua katika muonekano mzuri zaidi.
- - Limetengenezwa kwa uhodari na umakini wa hali ya juu na mafundi walio beboe katika kazi hiyo ili kulifanya liendane na hadhi ya Maqaam tukufu.
- - Limetengenezwa kwa vifaa imara ili kuhakikisha linakua imara na liweze kustahamili mazingira ya aina zote.
- - Limetumia karibu kilo (522) za madini ya fedha katika kutengeneza baadhi ya maeneo yake.
- - Limetumia karibu kilo (13) za dhahabu halisi.
- - Limetumia karibu kilo (2000) za madini ya kopa na karibu kilo (2500) za chuma imara pamoja na mbao za Swaaji na mbao zingine pamoja na aina zingine tofauti za madini.
- - Limenakshiwa kwa aya kutoka katika surat Nuur.
- - Limenakshiwa kwa beti za kaswida kutoka kwa mshairi bwana Ali Swafaar.
- - Linanakshi za mimea zilizo tengenezwa na mbunifu Dokta Amini Nuuriy.
- - Ndani ya dirisha hilo kumepambwa kwa mbao ya Swaaji na mbao zingine za rangi.
Fahamu kua dirisha tukufu la mazaru ya Qassim bun Imamu Kaadhim (a.s) limezinduliwa katika hafla iliyo fanyika ndani ya kiwanda cha Saqaa kinacho husika na kutengeneza madirisha na milango ya makaburi na mazaru tukufu siku ya Alkhamisi (6 Dhulhijja 1440h) sawa na (8 Agost 2019m).