Marjaa Dini mkuu ahoji mambo yanayo watesa raia wa Iraq

Maoni katika picha
Marjaa Dini mkuu amehoji maswali mengi katika khutuba ya pili ya swala ya Ijumaa leo (7 Dhulhijja 1440h) sawa na (9 Agost 2019m), iliyo swaliwa ndani ya ukumbi wa haram ya Imamu Hussein (a.s) chini ya uimamu wa Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, miongoni mwa maswali hayo ni: Je kuna njia ya kutatua shida zetu au hakuna?

Miongoni mwa mambo aliyo sema ni: Sisi kama raia wa Iraq, je kuna njia ya kutatua shida zetu au hakuna? Nilisema tazungumza kwa uwazi, je kuna njia? Je kuna mwanga? Je kuna muda maalum wa kutatua shida zetu au hakuna? Kwa nini tutabike daima? Kwa nini tuangaike daima? Haujafika wakati wa kupumzika? Wa kupewa haki za msingi za kila siku?

Akaongeza kusema kua: tutahangaika mpaka lini hadi vijana wanazeeka na watoto wanaota mvi bado shida zetu hazija tatuliwa!! Nini tatizo? Kwa kweli sisi tunashindwa kujibu maswali haya, lakini lazima tuongee, nini tatizo?

Akasema kua: watu wengi hawapati haki zao, kila wakati tunaambiwa zitaundwa sheria fulani yatatolewa maelekezo maalum, tunasubiri hatuoni kitu chochote kama tulivyo ambiwa, tunataka kuishi vizuri.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: