Kitengo cha utumishi chasambaza watumishi wake sehemu mbalimbali kwa ajili ya kuwahudumia mazuwaru wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) katika siku ya Arafa

Maoni katika picha
Sawa na vitengo vingine vinavyo shiriki kutekeleza mkakati wa kutoa huduma uliopangwa na uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu katika siku ya Arafa na Iddul-Adh-ha, kitengo cha utumishi kimesambaza watumishi wake sehemu zote za Ataba tukufu kwa ajili ya kuhudumia mazuwaru huku wakishirikiana na wahudumu wa kujitolea, ili kuhakikisha mazuwaru wanafanya ibaza kwa amani na utulivu.

Hiki ni kitengo kinacho toa kuduma za moja kwa moja kwa mazuwaru, kinafanya kazi mbalimbali, kama vile kuandaa na kuratibu sehemu za kuvulia viatu na kutunzwa (Kashwaniyya), kuandaa na kuratibu sehemu za kuweka vitu (Amanaat) sawa iwe ndani ya banda maalum au kwenye masanduku yaliyo wekwa kila mahala ndani ya haram tukufu, wanafanya kazi ya kutandika sehemu sehemu zilizo ongezwa katika haram kwa ajili ya mazuwaru, pia wameweka waelekezaji ndani ya haram tukufu, kwa ajili ya kutoa muongozo na maelekezo kwa mazuwaru watukufu.

Fahamu kua siku ya Arafa ni miongoni mwa siku maalum ambazo watu huja kwa wingu kufanya ziara kwa bwana wa mashahidi na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), pamboja na kufanya ibada maalum ya siku hiyo tukufu, jambo ambalo huhitajika nguvu ya ziada katika vitengo vya Atabatu Abbasiyya.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: