Kama kawaida yake katika kufanya kazi za kibinadamu na kutumikia watu kwa kushirikiana na taasisi za serikali na za kiraia, wafuasi wa kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji (Liwaau/26 Hashdi Sha’abi) katika mji wa Bashiri, wanaendesha zowezi kubwa la usafi katika mji huo, pamoja na kuosha (kudeki) barabara zote ikiwa kama sehemu ya kuwatumikia wananchi katika sikukuu ya Idul-Adh-ha.
Kiongozi wa zowezi hilo Ustadh Karaar Bashiri amesema kua: “Kazi hii ni miongoni mwa kazi za kujitolea kwa ajili ya kutumikia jamii, nayo ni muendelezo wa kazi nyingi zilizo fanywa na kikosi hiki katika mji wa Bashiri pamoja na miji mingine”.
Kwa kua ardhi ya mji huu imelowa damu za mashahidi wa kikosi cha Abbasi, akasema: “kazi hii inafanywa chini ya kauli mbiu isemayo: (tunafanya kwa jina la mashahidi), usafi umeratibiwa kwa kushirikiana na taasisi za serikali, tunasafisha barabara kuu tatu pamoja na lango la kuingia katika mji wa Bashiri na barabara zingine kubwa za mjini, ikiwemo barabara kubwa inayo elekea katika Husseiniyya ya Bashirul Muniir (s.a.w.w) na barabara kuu inayo elekea kwenye mtaa wa Zaharaa, pamoja na Husseiniyya na Bashirul Muniir na Shuhadaau Bashiir, tumeondoa uchafu kwenye njia zote”.
Kumbuka kua wapiganaji wa kikosi cha Abbasi (a.s) wanamchango mkubwa na muhimu katika mji wa Bashiri, mji huo ulikombolewa kwa utukufu wa mashahidi wa kikosi hicho na ujasiri wa wapiganaji wake, hivi sasa mji huo umerudi katika hali ya kawaida.