Atabatu Abbasiyya tukufu yaomboleza msiba wa rais wa chuo cha Al-Ameed

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu imeomboleza msiba wa rais wa chuo kikuu cha Al-Ameed kilicho chini ya kitengo cha malezi na elimu ya juu katika Ataba hiyo Dokta Jaasim Muhammad Marzuki aliye fariki wiki iliyo pita kutokana na maradhi ya ubongo, kwa kufanya majlis katika moja ya sehemu za uwanja wa katikati ya haram mbili zilizo pauliwa, na kuhudhuriwa na kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi pamoja na katibu mkuu Mhandisi Muhammad Ashiqar na jopo la wajume wa kamati kuu ya uongozi bila kuisahau familia yake na wapenzi wake kutoka ndani na nje ya mkoa wa Karbala pamoja na walimu na wanafunzi wa chuo cha Al-Ameed.

Majlisi ilidumu saa mbili, ilifunguliwa kwa Quráni tukufu kisha yakafuata mawaidha halafu wakamuomba Mwenyezi Mungu awape subira wanafamilia na wapenzi wa marehemu, na amuweke marehemu mahala pema peponi hakika yeye ni mwingi wa kusikia mwingi wa kujibu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: