Kwa picha: Kufunga sehemu za mwisho katika dirisha jipya la mazaru ya Sayyid Qassim bun Imamu Mussa Alkadhim (a.s)

Maoni katika picha
Mafundi wa kiwanda cha Saqaa kinacho husika na kutengeneza milango na madirisha ya kwenye makaburi na mazaru tukufu chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, wamemaliza kufunga sehemu za mwisho katika dirisha jipya la mazaru wa Qassim (a.s).

Mafundi wamefanya kazi saa (24) kwa ajili ya kuhakikisha wanamaliza haraka kufunga dirisha hilo lililo tengenezwa na mikono ya wairaq.

Kazi hiyo ilianza kwa kuondoa dirisha la zamani, kisha wakaweka majengo ya mbao yaliyo tengenezwa na idara ya mafundi selemala chini ya kitengo cha usimamizi wa kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu.

Baada ya hapo wakaanza kufunga taji la dhahabu, pamoja na kuweka maandishi ya Quráni na mashairi yaliyopo kati ya kibalaza cha msingi na nguzo za dirisha, kisha wakafunga vipande vya dirisha vilivyo tengenezwa kwa fedha.

Fahamu kua siku zijazo mazuwaru watashuhudia jambo la kihistoria la uzinguzi wa dirisha hilo jipya.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: