Kuanza kwa kongamano la tatu kwa wanafunzi wa shule za sekondari katika kituo cha utamaduni wa familia chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu

Maoni katika picha
Jumapili ya jana (16 Dhulhijja 1440h) sawa na (18 Agost 2019m) limeanza kongamano la tatu la wanafunzi wa sekondari linalo simamiwa na kituo cha utamaduni wa familia chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu kwa kushirikiana na ofisi kuu ya malezi katika mkoa wa Karbala.

Siku ya kwanza ilikua na mawaidha mbalimbali, mada ya kwanza ulihusu namna ya kuishi na watu ikafuatiwa na mada ya kifiqhi.

Kongamano litadumu siku tano mfululizo na linakusudia kuongeza uwelewa wa mambo ya kifiqhi, Aqida na mambo mengine.

Fahamu kua kituo kitakua na ratiba maalum ya Idul-Ghadiir katika siku ya pili na ya tatu ya kongamano hilo, washiriki wanaishi katika mazingira ya Idul-Wilayah ya kiongozi wa waumini Ali (a.s).

Kumbuka kua ofisi za kituo zipo Karbala/ mtaa wa Mulhaq/ barabara ya Hospitali ya Hussein (a.s) ndani ya jengo la kituo cha Swidiqah Twahirah (a.s), kinatoa huduma kwa wananchi wote wa Iraq hususan waishio Karbala, kwa mawasiliano zaidi piga simu namba (07828884555) namba hiyo inapatikana kwenye (Viber, Whatsapp na Telegram) pia unaweza kujiunga na kituo kwa kupitia link ifuatayo: https://t.me/thaqafaasria1.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: