Idul-Ghadiir, Idullahi Akbaru.

Maoni katika picha
Idu-Gadiir imeitwa (Idullahi Akbaru) kutokana na umuhimu wake, katika siku kama ya leo mwezi kumi na nane Dhulhijja mwaka wa kumi hijiriyya lilifanyika tukio kubwa na muhimu sana, kutokana na umuhimu wake Mwenyezi Mungu mtukufu alimwambia Mtume (s.a.w.w) awafikishie ujumbe waislamu katika eneo hilo (Ghadiir-Ghum), wala hakumuacha afike Madina, Mwenyezi Mungu mtukufu anasema: (Ewe Mtume fikisha uliyo teremshiwa kutoka kwa Mola wako Mlezi. Na ikiwa hukufanya hayo basi hukufikisha ujumbe wake. Na Mwenyezi Mungu atakulinda na watu. Hakika Mwenyezi Mungu hawaongoi watu makafiri).

Tukio hilo linaonyesha umuhimu wa hatua inayo fuata kwa waislamu, nafasi ya Uimamu, nafasi hiyo ndio inakamilisha kazi ya Utume.

Imeitwa Idullahi Akbaru kwa sababu siku hiyo ndio ilikamilika Dini na ikatimia Neema kutokana na kauli ya Mwenyezi Mungu isemayo: (Leo nimekukamilishieni Dini yenu na nimekutimizieni neema yangu, na nimekupendeleeni Uislamu uwe ndio Dini).

Pia imeitwa Idullahi Akbaru kwa sababu siku hiyo ilikamilisha Imani, kutokana na maneno ya Mwenyezi Mungu mtukufu: (Mabedui wamesema: Tumeamini. Sema: Hamjaamini lakini semeni: Tumesilimu. Kwani Imani haijaingia katika nyoyo zenu, na mkimtii Mwenyezi Mungu na Mtume wake, hatakupunguzieni chochote katika vitendo vyenu. Hakika Mwenyezi Mungu ni mwenye kusamehe, mwenye kurehemu).

Wilaya ndio inayokamilisha Imami, kama anavyo sema Mtume (s.a.w.w) kuhusu kiongozi wa waumini (a.s) katika vita ya Khandaq: (Imepigana Imani yote dhidi ya Ukafiri wote).

Na imeitwa Idullahi Akbaru kwa sababu Iddi zote husherehekewa na waislamu pamoja na wanafiki ispokua Idul-Ghadiir, haisherehekewi ispokua na muumini, kutokana na kauli ya mtume (s.a.w.w) isemayo: (Ewe Ali hatakupenda ispokua muumini na hatakuchukia ispokua mnafiki).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: