Kituo cha miradi ya Quráni kinafanya mashindano ya Quráni ya vikundi kwa wanafunzi wa mradi wa kiongozi wa wasomaji wa kitaifa

Maoni katika picha
Kituo cha miradi ya Quráni chini ya Maahadi ya Quráni tukufu katika Atabatu Abbasiyya kinafanya mashindano ya Quráni kwa wanafunzi wa mradi wa kiongozi wa wasomaji wa kitaifa, kwa kushiriki shule zote zilizopo kwenye mradi huo.

Mashindano haya ni moja ya ratiba za mradi inayo lenga kuendeleza vipaji vya washiriki na kuvionyesha kwa walimwengu sambamba na kuandaa vijana wanaoshikamana na kitabu cha Mwenyezi Mungu mtukufu.

Vimeshiriki vikundi nane, kila kikundi kina watu watano ambao wanasoma vitu tofauti na wanapita katika hatua tatu, kuna hatua ya mtowano katika usomaji wa mahadhi ya kiiraq na kimisri, hatua ya usomaji kwa kuigiza sauti ya wasomaji wakubwa wa Quráni na hatua ya maswali kuhusu maarifa ya Quráni kwa ujumla.

Fahamu kua mradi wa kiongozi wa wasomaji wa kitaifa awamu ya tano unavipengele vingi vinavyo lenga kuandaa msomaji mwenye kuelewa Quráni na masomo ya Aqida, Fiqhi, Akhlaq na adamu za usomaji wa Quráni, sambamba na kufanya hafla na kutoa mihadhara mbalimbali kuhusu Quráni tukufu na kizazi kitakatifu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: