Kukamilika kwa maandalizi ya kongamano la kwanza la amani ya jamii

Maoni katika picha
Kamati ya maandalizi ya kongamano la Amani ya jamii la kwanza linalo simamiwa na kitengo cha kulinda nidham katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imetangaza kukamilika kwa maandalizi yote, kongamano linatarajiwa kuanza siku ya Alkhamisi ijayo (27 Dhulhijja 1440h) sawa na (29 Agost 2019m) ndani ya ukumbi wa Imamu Hassan katika Atabatu Abbasiyya (a.s).

Kamati imesema kua kongamano litafanyika chini ya kauli mbiu isemayo (Amani ni salam ya mila yetu na amani ni dhima yetu) linalenga kujenga uzalengo kwa wananchi, ukizingatia kua ni jukumu la kila mtu hususan kwenye miji mitukufu inayo pokea mazuwaru kila wakati ndani ya mwaka mzima, kongamano hili linaangazia kazi zilizo fanywa na watafiti katika sekta hii, kwa ajili ya kuondoa matatizo yaliyopo katika jamii ya wairaq na katika maeneo matakatifu, kwa kufuata tafiti za kielimu na kuondoa muonekano hasi.

Kongamano litakua na uwasilishwaji wa mada za kitafiti kuanzia katika kikao cha ufunguzi hadi cha ufungaji na kujadili vipengele vya maafa, watashiriki watafiti wa kidini na kisekula walio bobea katika mambo hayo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: