Kaswida iliyo dumishwa na washairi: (Ewe mwezi wa Ashura hakuna mwezi wa mfano wako) kaswida ambayo husomwa katika kila msimu wa huzuni za Ashura

Maoni katika picha
Haikua kudumu kwa shairi lake, ispokua ni katika neema za harakazi za Husseiniyya ambazo Mwenyezi Mungu mtukufu ametaka zidumu milele na milele, na anamdumisha kila atakaye fuata mwenendo wake na nyayo za mbora wa mashahidi na bwana wa vijana wa peponi Imamu Hussein (a.s).

Alipokua akifuata nyayo za Imamu Hussein (a.s) na kushiriki maombolezo ya Ashura, mshairi wetu marehemu Shekh Yasini Kuufi (aliyekufa zaidi ya miaka hamsini na sita iliyo pita) alikua mshairi maarufu aliye julikana kwa kuandika mashairi ya Husseiniyya, yanayo amsha hisia za huzuni katika nafsi za wapenzi wa Ahlulbait (a.s), katika miaka ya arubaini karne iliyo pita hadi miaka ya themanini, aliandika kaswida zilizo tamba sana wakati huo na bado zinaendelea kusomwa na waombolezaji wa Ashura hadi sasa.

Miongoni mwa kaswida hizo ni (Ewe mwezi wa Ashura hakuna mwezi wa mfano wako), iliyo somwa jana katika shughuli ya kubadilisha bendera ya kubba la Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) kama tangazo la kuanza kwa msimu wa huzuni, shairi hilo linasema:

Ewe mwezi wa Ashura hakuna mwezi wa mfano wako

Kwako Abu Sajjaad alitoa dalili zake.

Ewe mwezi wa Ashura umeamsha huzuni

Kwako mwili wa Hussein ulikaa bila kuzikwa.

Hussein katutoka machozi yabubujika usoni

Umeumia moyo wa Mtume mbora wa viumbe.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: