Hussein alimwambia: Abu Thamama Swaidiy (Umekumbuka swala.. Mwenyezi Mungu akujaalie kua miongoni mwa wanaoswali na wakumbushao)

Maoni katika picha
Abu Thamama Amru bun Abdullahi Swaidiy mkumbushaji wa swala, alikua katika wafuasi wa bwana wa mashahidi (a.s), na katika wanajeshi wake wakweli walio uwawa mbele yake katika vita ya Twafu, jina lake limebakia katika kurasa za historia ya kiislamu kama kamanda mwenye mapenzi makubwa sana kwa Imamu wa zama zake.

Jemedari huyo (r.a) ndiye aliye kumbusha swala katikati ya vita, akamwambia Imamu Hussein (a.s) kua yupo tayali kufa kishahidi kwa ajili yake baada ya kuswali Adhuhuri, Imamu (a.s) akamwambia: (Umekumbuka swala.. Mwenyezi Mungu akujalie kua miongoni mwa wanaoswali na wakumbushao, ndio huu ni mwanzo wa muda wake).

Wapenzi wa Imamu Hussein (a.s) wako hivyo kila mahala na muda wote, huadhimisha alama za Mwenyezi Mungu na kutekeleza ibada zake, hata kama wakiwa karibu na kifo, baba wa watu huru hakutoka ispokua kwa ajili ya kuwafanya watu waendelee kufanya ibada walizo amrishwa na Mwenyezi Mungu mtukufu na kuhimizwa na Mtume Muhammad (s.a.w.w).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: