Atabatu Abbasiyya tukufu kimefungua (#Ashura_mwenendo) kwa ajili ya kurushia habari katika mwezi wa Muharam…

Maoni katika picha
Kutokana na kuingia kwa mwezi wa huzuni, mwezi wa Muharam, Malaika hukunjua mbawa zao kwa ajili ya huzuni ya msiba wa watu wa nyumba ya Mtume (s.a.w.w), mtandao wa kimataifa Alkafeel ambao ni mtandao rasmi wa Atabatu Abbasiyya tukufu umefungua (#Ashura_mwenendo), itakayo tumika katika mambo yote ya urushaji wa habari za luninga, mitandao ya kijamii (facebook, twitter na instagram) za Ataba tukufu.

Jambo hili linafanyika kwa mwaka wa kwanza ili kurahisisha zaidi urushaji wa habari katika msimu huu wa kuomboleza, na kufikisha harakati na mambo yanayo fanyika Karbala kwa watu wengi zaidi, ikiwa ni pamoja na kurahisisha utafutaji wa habari hizo kwa kila anayetaka kuishi katika mazingira ya Ashura, sawa iwe kwa kufuatilia habari za video au picha kutoka sehemu inayo aminika, kwa kutumia anuani stahiki kwa kila mada.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: