Kwa ukubwa unaokadiriwa kuwa mita za mraba (5000): Haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) imetandikwa busati jekundu

Maoni katika picha
Miongoni mwa majukumu ya kitengo cha usimamizi wa haram katika mwezi wa Muharam ni kutandika mazulia mekundi kwenye ukumbi wa haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s) katika eneo linye ukubwa unaokadiriwa kua mita za mraba (5000).

Kiongozi wa idara ya haram katika kitengo hicho Ustadh Jasim Muhammad Kadhim ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Kitengo cha usimamizi wa haram katika kila mwezi wa Muharam hutandika mazulia mekundu kwenye eneo linalo kadiriwa kua mita za mraba (5000) ndani ya haram tukufu, kwa ajili ya kulinda sakafu ya haram tukufu na kurahisisha upitaji wa mawakibu na mazuwaru”.

Akaongeza kua: “Tumechukua mazulia katika magodauni ya Atabatu Abbasiyya yaliyopa katika eneo la Ibrahimiyya, baada ya kuainisha ukubwa wa eneo linalo takiwa kutandikwa, kabla ya kutandika tulitanguliza nailoni kisha ndio tukatandika, mwaka huu tunatarajia kubakiza mazulia mekundu hadi tutakapo maliza matembezi ya tuwaleji”.

Fahamu kua kitengo cha usimamizi wa haram ni sawa na vitengo vingine vya Ataba tukufu, kinatumia nguvu zote katika kuwapokea na kuwahudumia mazuwaru na waombolezaji katika kipindi chote cha huzuni kwa watu wa nyumba ya Mtume (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: