Ilitokea siku kama ya leo mwezi saba Muharam mwaka 61h: Imamu Hussein (a.s) azuiliwa maji.

Maoni katika picha
Mchana wa mwezi saba Muharam mwaka 61h, Omari bun Saadi (laana iwe juu yake) aliweka askari mia tano kulinda mto wa Alqamiy, baada ya kupokea barua kutoka kwa ibun Ziyadi ikimtaka amzuwie Imamu Hussein (a.s) na watu wake kutumia maji.

Siku hiyo pia Imamu Hussein (a.s) alikutana na Omari bun Saadi na kujadiliana naye kuhusu kutowashambulia Ahlulbait (a.s), Omari hakukubali kuacha vita, Imamu Hussein (a.s) akamwambia: (Mwenyezi Mungu akuchinje kitandani kwako haraka wala hatakusamehe siku ya ufufuo, wallahi mimi naamini hautakula ngano za Iraq ispokua kidogo).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: