Juhudi kubwa zinafanywa na kitengo cha kulinda nidham katika kutekeleza mkakati maalum wa kuimarisha usalama siku ya Ashura.

Maoni katika picha
Kitengo cha kulinda nidham katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimeanza kutekeleza mkakati maalum wa kuimarisha usalama usiku na mchana wa mwezi kumi Muharam, kwa ajili ya kuhakikisha usalama wa mazuwaru na kuratibu matembezi yao.

Kitengo kinatumia watumishi wake wote kutekeleza mkakati wa kuimarisha usalama ulio wekwa na vyombo vya ulinzi na usalama pamoja na kikosi cha kulinda malalo mawili matukufu, sambamba na mamia ya watu wanaojitolea kusimamia uingiaji na utokaji wa mazuwaru katika milango ya haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s), na kuweka mazingira mazuri ya kufanya ibada ya ziara kwa amani na utulivu ndani ya haram tukufu, pamoja na kuratibu uingiaji na utokaji wa mawakibu za waombolezaji na makundi ya mazuwaru wanao tarajiwa kufurika katika haram hiyo takatifu.

Fahamu kua kitengo cha kulinda nidham sawa na vitengo vingine vya Atabatu Abbasiyya tukufu, kimetumia uwezo wake wote katika kuwatumikia mazuwaru wa bwana wa mashahidi na ndugu yake mnyweshaji wenye kiu Karbala (a.s), katika ziara hii na zingine.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: