Ilitokea siku kama ya leo mwezi tisa Muharam 61h: Kuwasili kwa barua ya ibun Ziyadi aliyo amrisha kuuliwa Imamu Hussein (a.s) na kuzingira hema zake

Maoni katika picha
Katika siku kama leo mwezi tisa Muharam 61h, aliwasili mal-uuni Shimri akiwa na barua ya Ubaidu-Llahi bun Ziyadi aliyo muandikia Omari bun Saadi, isemayo: Mimi sijakutuma kwa Hussein ukawe ngao yake, kujadiliana naye, kumpa Amani, au kumuombea msamaha, kama Hussein na wafuasi wake wakila kiapo cha utii kwangu walete kwa amani, na kama wakikataa wauwe na usulubu miili yao, hakika wanastahiki kufanyiwa hivyo, ukimuua Hussein kanyaga kanyaga kifua chake kwa farasi..

Alipo soma, akamuambia: Una nini? Mwenyezi Mungu asiikuubishe nyumba yako, Allah halipendi jambo ulilo niletea, wallahi Hussein hatasalim (hatatoa kiapo cha utii) hakika yeye ni mtukufu, Shimri akasema: niambie utafanya nini.. tekeleza amri ya kiongozi wako kama hautaki niachie mimi tatekeleza, akasema: hapana.. sikuachii wewe, tatekeleza mimi mwenyewe na wewe ongoza jeshi la watembea kwa miguu..

Siku hiyo hiyo wakazingira hema za Abu Abdillahi (a.s), imepokewa kutoka kwa Abu Abdillahi Swadiq (a.s) anasema: (Mwezi tisa ndio siku aliyo zingirwa Imamu Hussein –a.s- na wafuasi wake –r.a- Karbala, wapiganaji wa Sham walikusanyika, bun Marjana na Omari bun Saadi wakafurahi kwa kuwa na wapiganaji wengi, wakamdhalilisha Hussein –a.s- na wafuasi wake –r.a- wakajua kua hakuna watu watakao kuja kumsaidia Hussein –a.s- kwani yupo ugenini na hana watu watakao msaidia).

Kisha akasema: (Siku ya Ashura ndio siku aliyo uwawa Hussein –a.s- katikati ya maiti za wafuasi wake, hivi funga inakua (sunna) katika siku hiyo?!! Hapana, namuapa Mola wa baitul-haraam hiyo sio siku ya kufunga bali ni siku ya huzuni na msiba, waliopata viumbe wa mbinguni na ardhini pamoja na waumini wote, ni siku ya furaha kwa ibun Marjana na Aali Ziyadi na watu wa Sham –Mwenyezi Mungu amewakasirikia na vizazi vyao- atakaye funga katika siku hiyo atafufuliwa na Aali Ziyadi akiwa amekasirikiwa, atakaye sherehekea siku hiyo Mwenyezi Mungu ataingiza unafiki katika moyo wake mpaka siku ya kiyama, ataondolewa baraka yeye na watu wa nyumbani kwake, atashirikiana na shetani katika kila kitu).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: