Maukibu ya kuomboleza: Masayyid ambao ni watumishi wanaomboleza msiba wa babu yao Imamu Hussein (a.s) na Ahlulbait (a.s) pamoja na wafuasi wake.

Maoni katika picha
Kama kawaida yao kila mwaka siku kama ya leo usiku wa mwezi kumi Muharam, Masayyid ambao ni watu wanaotokana na kizazi cha Mtume Muhammad (s.a.w.w) wanao fanya kazi katika Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, pamoja na Masayyid ambao sio wafanya kazi katika Ataba hizo wameshiriki katika maukibu ya pamoja kwa ajili ya kuomboleza kifo cha Imamu Hussein (a.s) na Ahlulbait na wafuasi wake (a.s), mbele ya malalo yake na malalo ya mbeba bendera Abulfadhil Abbasi (a.s).

Matembezi ya maukibu hiyo ambayo washiriki wake walivaa nguo maalum, yalianzia barabara ya Kibla ya Abulfadhil Abbasi (a.s), na kuelekea katika malalo yake tukufu, kisha katika malalo ya bwana wa mashahidi Imamu Hussein (a.s), wakipitia kwenye uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu.

Kumbuka kua maukibu ya Masayyid ni miongoni mwa maukibu za kihistoria katika mji wa Karbala, ilianzishwa baada ya kuanza taifa la Iraq mwaka (1921m), imeendelea kuwepo na kuongezeka mwaka baada ya mwaka, maukibu hii pamoja na waombolezaji wengine walipigwa marufuku na utawala ulio pita, marufuku hiyo iliendelea hadi utawala huo ulipo ondolewa madarakani mwaka (2003m), shuguli za kuomboleza zikarudi kama ilivyo kua zamani, kila mwaka ufikapo mwezi kumi Muharam maukibu hii hufanya matembezi, inahusisha familia za Masayyid walio wahi kufanya kazi katika Ataba mbili tukufu, pamoja na wanaofanya kazi hivi sasa kwenye Ataba hizo (Husseiniyya na Abbasiyya).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: