Pamoja na msongamano mkuwa: Wafanya kazi wa kitengo cha utumishi wanaendelea kudumisha usafi

Maoni katika picha
Idara ya usafi chini ya kitengo cha utumishi katika Atabatu Abbasiyya tukufu, inaendelea na kazi ilizo pangiwa katika siku za Ashura, ambazo imeanza kuzifanya tangu Muharam mosi, wanafanya kila wawezalo katika kutekeleza wajibu wao wa kudumisha usafi katika maeneo yote yanayo zunguka haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s).

Kazi zinazo fanywa na watumishi wa idara hii pamoja na watu wanao jitolea waliopo kila sehemu, wanaendelea kutoa uchafu kila kona na kuuweka katika gari maalum za taka, sehemu ambazo gari hazifiki wanabeba na kupeleka sehemu ambazo zinafikika na gari hizo, kazi hiyo inafanywa usiku na mchana, itaendelea hadi baada ya ziara.

Kumbuka kua kitengo cha utumishi katika Atabatu Abbasiyya ni miongoni mwa vitengo vinavyo wahudumia mazuwaru moja kwa moja, na hufanya kazi kwa bidii na umakini mkubwa, ndani na nje ya Ataba, kitengo hicho kina idadi kubwa ya wafanyakazi wa kujitolea wanao shirikiana bega kwa bega katika kuwahudumia mazuwaru.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: