Maahadi ya Quráni tukufu yahuisha usiku wa mwezi kumi Muharam kwa kusoma Quráni ndani ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s)

Maoni katika picha
Miongoni mwa harakati zake maalum za kuhuisha usiku wa Ashura, Maahadi ya Quráni tukufu chini ya Atabatu Abbasiyya imehuisha usiku wa mwezi kumi Muharam kwa kusoma Quráni ndani ya haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s).

Thawabu za kisomo hicho zimeelekezwa kwa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) pamoja na wafuasi wake watukufu, katika kisomo hicho wameshiriki pia mazuwaru waliokuja kufanya ibada usiku huu, Maahadi imegawa juzuu za Quráni kwa mazuwaru hao, waliokesha wakisoma Quráni, wakiswali na kusoma dua.

Kumbuka kua Maahadi ya Quráni tukufu chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinadamu katika Atabatu Abbasiyya inaratiba kamili ya mwezi wa Muharam na Safar, na jambo hili ni miongoni mwa ratiba zake maalum.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: