Ugeni kutoka Atabatu Abbasiyya tukufu unafanya maombolezo ya Ashura katika mji wa Samaraa

Maoni katika picha
Kwa maelekezo ya kiongozi mkuu wa kisheria wa Atabatu Abbasiyya tukufu Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, na kwa kushirikiana na uongozi mkuu wa Atabatu Askariyya, jana mwezi kumi Muharam mwaka (1441h) sawa na (10 Septemba 2019m) ugeni kutoka Atabatu Abbasiyya umeelekea katika malalo ya maimamu wawili Askariyyain (a.s), kuomboleza mauwaji ya Twafu kwa mwaka wa pili mfululizo, wakishirikiana na Atabatu Kadhimiyya na msikiti wa Aali Yasiin uliopo katika mji wa Kadhimiyya.

Ugeni huo ulihusisha wafanyakazi wa Ataba tukufu pamoja na wapenzi wa Ahlulbait (a.s) kutoka Karbala na mikoa mingine ya Iraq, walikua zaidi ya mazuwaru elfu tano.

Mjumbe wa kamati kuu ya uongozi katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Mustwafa Murtadha Dhiyaau-Diin ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Kwa maelekezo ya kiongozi mkuu wa kisheria sayyid Ahmadi Swafi tumefanikiwa kuandaa ratiba ya maombolezo kwa mwaka wa pili mfululizo katika mji wa Samaraa, tukiwa na idadi kubwa ya wapenzi wa Ahlulbait kutoka Karbala na mikoa mingine (Bagdad, Diyala, mji wa Tuzkhumato na mikoa ya kaskazini mingine) kwa ajili ya kuomboleza siku ya kumi na usiku wa mwezi kumi na moja Muharam”.

Sayyid Dhiyaau-Diin akaongeza kua: “Tulianza kwa kufanya maombolezo ya pamoja na kuelekea katika nyumba ya Imamu msubiriwa (a.f) kisha tukasoma maqtalu ya Imamu Hussein pamoja na kusoma ziaratu-Ashura, baada ya swala ya Dhuhurain tukakamilisha ratiba kwa kutembea umbali wa kilometa moja, kisha tukaelekea katika malalo ya Maimamu wawili Askariyyain (a.s) kwa ajili ya kutoa pole kwa Imamu msubiriwa (a.f), halafu tukasoma ziyaratu-Naahiyyah kabla ya swala ya Magharibi na Isha”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: