Wafanyakazi wa Atabatu Abbasiyya tukufu wameanza kufanya kazi ya usafi

Maoni katika picha
Wafanyakazi wa kitengo cha utumishi katika Atabatu Abbasiyya tukufu wameanza kufanya kazi ya usafi katika barabara na sehemu zinazo zunguka haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s) baada ya kumaliza ziara ya Ashura.

Makumi ya wafanyakazi wa kitengo cha utumishi wameanza kusafisha eneo la katikati ya haram mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya pamoja na sehemu zinazo zunguka haram hizo, sambamba na kutandua zulia jekundu, wakiwa pamoja na idadi kubwa ya watu wanao jitolea, wamefanikiwa kurudisha eneo hilo katika hali ya kawaida ndani ya muda mfupi.

Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya tukufu hufanya usafi mkubwa kila baada ya kumaliza ziara kubwa kwa ajili ya kurudisha hali ya kawaida katika haram tukufu na maeneo jirani.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: