Kwa maelekezo ya kiongozi mkuu wa Kisheria: Atabatu Abbasiyya tukufu yatuma ujumbe kwenda kuangalia watu waliojeruhiwa katika matembezi ya Towariji

Maoni katika picha
Asubuhi ya leo mwezi (11 Muharam 1441h) sawa na (11 Septemba 2019m) ujumbe wa Atabatu Abbasiyya umekwenda kuwaangalia watu walio jeruhiwa katika msongamano wa matembezi ya Towariji yaliyo fanyika mwezi kumi Muharam, na kulazwa katika hospitali ya Zainul-Aabidina, hospitali ya Alkafeel pamoja na hospitali ya Husseiniyya katika mji mtukufu wa Karbala, ujumbe huo umewasilisha salamu za kiongozi mkuu wa kisheria Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi kwa majeruhi pamoja na familia zao, na kuwaombea dua ya kupana haraka.

Ujumbe huo umehusisha wanachuoni wa Ataba tukufu na Masayyid pamoja na watumishi na kuongozwa na Mheshimiwa kiongozi mkuu wa Atabatu Husseiniyya Shekh Abdulmahdi Karbalai, wamewatembelea majeruhi waliolazwa na kuangalia maendeleo ya tiba zao baada ya kuumia katika tukio hilo la kusikitisha.

Atabatu Abbasiyya tukufu ilitangaza kua ipo tayali kuwasaidia kila kitu katika matibabu yao.

Fahamu kua uongozi mkuu wa Ataba mbili Husseiniyya na Abbasiyya umesha tangaza kufanya kisomo cha kuwarehemu mashahidi wa matembezi ya Towariji, katika uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu siku ya Jumamosi (14 Muharam 1441h) sawa na (14 Septemba 2019m) kuanzia saa tisa hadi saa kumi na mbili Alasiri.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: